Mechi ya Dabi ya Kariakoo leo imemalizika kwa sare ya 2-2 kati ya Simba SC na Yanga SC katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo. Magoli ya Simba yamefungwa na Libasse Guèye na Clatous Chama , huku Yanga wakirudi mchezoni kupitia kwa Prince Dube na Bakari Mwamnyeto . Simba SC walianza kwa kasi ya juu na presha ya mapema, wakitumia mashambulizi ya haraka kuvunja safu ya ulinzi ya Yanga. Ndani ya dakika 10 za mwanzo, wekundu wa msimbazi walikuwa tayari mbele kwa mabao mawili kupitia kwa Guèye (3’) na Chama (10’), hali iliyoonyesha ufanisi wao katika transitions za haraka na kutumia makosa ya mpinzani. Yanga SC walipunguza kasi hiyo kupitia kwa Prince Dube (18’), bao lililotokana na mpango wa haraka uliovunja pressing ya Simba. Bao hilo lilibadili mwelekeo wa mchezo, ambapo Yanga walianza kupata control ya kiungo na kupunguza utawala wa Simba katika maeneo ya mbele. Kipindi cha pili kilionyesha tofauti ya wazi ya mbinu ( tactical approach ). Yanga walidhibiti zaidi umiliki wa mpi...